Condoleezza Rice aitahadharisha Korea ya kaskazini na mradi wake wa kinuklea
6 Januari 2007Matangazo
Washington:
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice ameionya Korea ya kaskazini dhidi ya kufanya jaribio la pili la silaha za kinuklea.Baada ya mazungumzo pamoja na waziri mwenzake wa Korea ya kusini,Song Min Soon mjini Washington,bibi Condoleezza Rice amesema jaribio kama hilo litaifanya izidi kutengwa nchi hiyo ya kikoministi katika majukwaa ya kimataifa.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Korea ya kusini Song Min Soon amesisitiza haoni kama kuna ikshara ya Korea ya kaskazini kufanya jaribio jengine la silaha zake za kinuklea.Waziri wa mambo ya mnchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice ameelezea matumaini ya kuona mkutano wa pande sita kuhusu mradi wa kinuklea wa Korea ya kaskazini ukiitishwa upya hivi karibuni.