1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congo: Ugonjwa usiojulikana ni aina mpya ya Malaria

17 Desemba 2024

Wizara ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema ugonjwa ambao haukuwa unajulikana uliokuwa umesambaa katika eneo la Panzi ni aina kali ya ugonjwa wa Malaria.

https://p.dw.com/p/4oGDV
Kongo Kinshasa 2024 | Gesundheitsminister Kamba bei Pressekonferenz zur Krankheitslage
Waziri wa afya wa Kongo Roger Kamba anahudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, Kongo, Alhamisi, Desemba 5. 2024Picha: Samy Ntumba Shambuyi/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, wizara hiyo imesema hatimaye imefahamu ugonjwa uliokuwa unawaangamiza wengi kwa kasi na kuthibitisha kwamba ni aina kali ya Malaria inayoathiri mfumo wa kupumua na kufanya mwili kudhoofika zaidi kufuatia utapiamlo. Wizara hiyo pia imesema visa 592 vimeripotiwa tangu mwezi Oktoba mwaka 2020 huku kiwango cha vifo kikifikia asilimia 6.2 Mapema mwezi huu, serikali katika eneo hilo ilisema watu 143 walikufa kutokana na ugonjwa huo Kusini Magharibi mwa mkoa wa Kwango mwezi Novemba.