1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CORD yakataa kuundwa kamati ya Bunge

Isaac Gamba10 Juni 2016

Upinzani Kenya haukubaliani na mpango wa rais Uhuru Kenyatta kuutafutia suluhu mzozo wa Tume ya Uchaguzi IEBC na kusema maandamano ya kuipinga Tume yatafanyika kila Jumatatu na Ijumaa.

https://p.dw.com/p/1J4UE
Waandamanaji wa upinzani Kenya
Picha: DW/A. Kiti

[No title]

Pande mbili za kisiasa nchini Kenya za CORD na Muungano wa Jubilee zikiendelea kuvutana kuhusiana na kile kinachoelezwa kutokuwa na imani na tume ya kusimamia uchaguzi wa mwakani nchini humo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa kwa upande wao wanatoathimini juu ya mwelekeo wa kisiasa katika kuelekea uchaguzi huo wa mwakani. Baron Shitemi ni mmoja wa wachambuzi hao wa masuala ya kisiasa na amezungumza na Isaac Gamba wa DW.