DARESALAAM:Mazungumzo juu ya utekelezaji wa mkataba wa amani ya Burundi wacheleweshwa
9 Juni 2005Mazungumzo juu ya utekelezaji wa mkataba wa amani kati ya serikali ya Burundi na kundi la waasi la FNL yalicheleweshwa hapo jana baada ya wawakilishi wa waasi kushindwa kufika kwenye mazungumzo hayo.
Afisa mmoja wa Tanzania aliliambia shirika la habari la AFP kwamba ujumbe wa serikali ya Burundi umefika lakini wawakilishi wa FNL hawakutimia kwa hiyo ilibidi kuwasubiri wenzao.
Rais wa Burundi Domitien Ndayizeye na kionmgozi wa waasi hao Agathon Rwasa walitia saini makubaliano ya kumaliza vita vilivyoyagharimu maisha ya watu laki tatu nchini Burundi.
Viongozi hao walikubaliana kuunda tume katika kipindi cha mwezi mmoja,itakayoweza kutekeleza mkataba huo wa amani.
Licha ya kutiwa saini kwa makubaliano ya amani kundi la FNL linashutumiwa kwa kuendeleza mashambulizi dhidi ya raia na kujaribu kuvuruga uchaguzi wa madiwani uliofanyika hivi karibuni.