1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dawa ya njaa Afrika

Mohamed Dahman26 Machi 2013

Inaelezwa kwamba iwapo Afrika inataka kukomesha njaa lazima iandae mpango rahisi kwa wakulima milioni 900 ambapo kuna uwezekano wa kuongezeka kwa mapato ya wakulima kwa asilimia 80.

https://p.dw.com/p/184Xp
Vor allem Deutschland importiert die zuckersüßen Bio-Ananas aus Uganda. Bei der Biomesse "Biofach" in Nürnberg waren im Februar allein 13 Vertreter aus Uganda in Deutschland. Copyright: DW/Ludger Schadomsky 07.03.2013, Kampala, Uganda
Nanasi UgandaPicha: DW/L. Schadomsky

Jambo hilo linafanya gharama za uzalishaji zinatakiwa ziwe zimepunguzwa kwa kiwango kikubwa sana

"Tizameni kule" anatamka hayo Vincent Ssoko akimaanisha kule kwenye majani ya kijani ya migomba ambayo haitamaniki .ikiyumba kutokana na kipepo cha joto ikiwa imezungukwa na senyen'ge.Anasema "Daima nimekuwa nikiwambia jirani yangu kwamba fanya kama nilivyofanya mimi.Chimba shimo kubwa ili kuufanya mti huo uwe na nafasi ya kutosha,jaza mbolea ya kutosha na uhakishe kwamba mbegu hazipandwi kwa kukaribiana."Jirani huyo anananuwa tena mbolea ya ghali na kufidia mavuno mabaya.

Vincent Ssoko mkulima wa bio(anayetumia ukulima wa asili bila ya kemikali) huko Busana katika mkoa wa Kayunga ambapo huchukuwa kama saa tatu kwa mwendo wa gari kutoka kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala ana sababu nzuri ya kutabasamu.Kwani alikuwa ndio kwanza amenenuwa tena hekta 20 za ardhi ziada ya hekta 29 alizokuwa nazo. Anasema hapo mwaka 1998 alianza na hekta tatu. Mkulima huyo mwenye umri wa miaka 46 hivi sasa anaotesha mananasi, ndizi, kahawa na maharage kwa njia ya bio... na hasa kwa kuwa na cheti cha bio.Kwa hiyo anaweza kusafirisha mazao yake hayo katika soko la bara la Ulaya. Anaonyesha kwa fahari manasi matamu yalioteshwa kwenye mstari mrefu ulionyooka.Zaidi ya nusu ya matunda 700,000 kwa mwaka yanakwenda Ujerumani.Ssoko hujipatia shilingi 700 za Uganda sawa na senti 20 za euro kwa tunda moja.Katika soko la ndani ya nchi huwa anajipatia tu shilingi 150 tu sawa na centi nne za euro.

Ongezeko la 80% la mapato ya mazao ya bio

Iwapo Afrika inataka kukomesha njaa lazima iandae mpango rahisi kwa wakulima milioni 900: Ni dhahiri kwamba mapato lazima yaongezwe na wakati huo huo gharama za uzalishaji hazina budi kupunguzwa kwa kiwango kikubwa sana.Uchunguzi kabambe uliofanywa na Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) hapo mwaka 2010 umedokeza kwamba mambo yanakwenda vizuri : Uchunguzi miongoni mwa mashamba milioni kumi na mbili takriban katika nchi 60 zinazoendelea umebaini kwamba wastani wa mapato huongezeka kwa hadi asilimia themanini wakati konde zinapolimwa kwa misingi ya ekolojia.Uganda ilioko Afrika Mashariki ni aina ya maabara ya majaribio.Vincent Ssoko anasema badala ya kununuwa madawa yalio ghali anatumia mbolea ya asili anayoipata bure kutokana na wanyama wake na kwamba badala ya kutumia madawa ya kuulia wadudu anatumia mkojo na majivu kupambana na wadudu hao waharibifu wa mazao.Kwa kazi ya kun'gowa magugu pekee mkulima huyo inabidi amlipe mtu,kwani hapa pia ni marufuku kutumia madawa ya kuuwa magugu.

Die Rechnung geht auf: Mehr Bio = höherer Ertrag = höheres Haushaltseinkommen = Diversifizierung und höhere Nährstoffaufnahme Copyright: DW/Ludger Schadomsky 07.03.2013, Kampala, Uganda
Mkulima wa Uganda akihesabu fedhaPicha: DW/L. Schadomsky

Bio kwa watu wote

Katika mji mkuu wa Kampala Judith Nabatanzi akiwa mwenye motisha anapiga chapa kwa kutumia kompyuta yake.Judith na mwenzake Cathy Kyazike wanaongoza kwa pamoja '' Duka la Mazao ya Kilimo Asilia '' - au "Nunua Mazao ya Kilimo Asilia ''.Ni jina la mradi wa duka hilo dogo ambalo lina mazao ya matunda na mboga mboga za aina mbali mbali yaliyozalishwa kwa utaratibu wa kilimo asilia kuanzia vikonyo vya vanila hadi karoti.Duka hilo linamilikiwa na Nogamu shirika mama la wakulima wanaofuta utaratibu wa kilimo asilia nchini Uganda na ni duka pekee la matunda na mboga mboga za bio zenye kuzalishwa kwa utaratibu wa asili nchini Uganda nchi yenye idadi ya watu miloini 35.

Kuanzia saa moja asubuhi Judith tayari anakuwa dukani kushughulkia oda za wateja wake.Anasema Ijumaa ni ndio siku kuu ya biashara katika kipindi cha wiki kutokana na kwamba wengi wa wateja wao wanataka kupika mwishoni mwa juma. Kwa hiyo inabidi wafunge vikapu vya mahitaji ya wateja takriban arobaini au hata zaidi,wakati huo wakulima waliowasili mwanzo wakiwa wameegesha kwenye mlango wa duka hilo na Boda Boda yaani taxi za pikipiki kama zinavyojulikana nchini Uganda.Siku moja kabla wakulima huwa wanazungumza kwa njia ya simu na Judith na Cathy kuwapa bei za mazao yao, asubuhi inayofuata wakulima huleta mazao yao dukani kwa kuondoka kutoka maeneo ya ndani mashambani na mapema kuepuka msongamano wa magari.

Shamba la Ssozi Muwangwa liko kama kilomita 30 magharibi kutoka Kampala. Mkulima huyu huyapakia maboksi yake ya nyanya kwenye pikipiki na anakwenda kwenye duka hilo mara moja kila wiki tokea mwaka 2007.Anaona bei za hapo ni nzuri kuliko bei za mazao ya kawaida yaani shilingi elfu nne sawa na euro moja centi kumi na tano kwa kilo ambayo ni bei nzuri zaidi kuliko ile ilioko kwenye soko la barabarani.Je inamaanisha kwamba anaweza kuthibitisha utafiti wa shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwamba mapato yanayotokana na mazao ya bio ni ya juu? Akiunga mkono uchunguzi huo wa UNEP Muwangwa anasema inakuwa ni kawaida kwa ardhi kuwa na rutuba bila ya kutumiwa kwa madawa ya kemikali na wanazalisha kwa wingi tena kwa kipindi kirefu pamoja na kuepuka ughali wa mbolea. Kwa jumla hujipatia mapato makubwa ya asilimia 30 na mara nyengine hata hamsini.

Wakati Muwangwa anapopakuwa maboxi yake Judia na Cathy huchambuwa oda zao na kutumbukiza kwenye vikapu matunda na mboga mboga mbali mbali kuanzia saladi, matufaa na karoti.Juu ya vikapu hivyo huwekwa karatasi za oda ili kuepusha mparaganyiko. Mbali ya Boda Boda pia kunakuwepo na magari yenye vipoza joto kwa ajili ya kuchukuwa vitu vinavyoweza kuharibika haraka vinaposafirishwa wakati wa asubuhi kutokana na joto lenye unyevu.

Wakulima wachache wa bio wana avyeti

Moses Muwanga anasema utaratibu wa kupata cheti cha bio kwa wakulima una gharama kubwa sana.Anakiri kwamba amesaidiwa na Nogamu chama cha wakulima wa Bio wenye kutumia kilimo asilia kugharamia cheti chake lakini wakulima wengi bado wanashindwa kuvilipia vyeti hivyo .Bei ya cheti hicho ni dola 24,000.(Muwanga anakunywa fundo moja la chai yake yenye cheti cha bio wakati akitafakari mahesabu hayo.)Muwanga ambaye ni kiongozi wa Nogamu kwenye ukuta wa ofisi yake kumetundikwa vyeti vya wteja wake kutoka Japani,Marekani na Umoja wa Ulaya ambao wote hao hao wametowa leseni kwa bidhaa za chama cha wakulima wa Bio nchini Uganda ,Nogamu.Kwa mujibu wa Muwanga ziara za wakaguzi hugharimu dola elfu nane.Zinahitajika elfu kumi na sita kubadili uoteshaji wa mazao wa kawaida na kuingia kwenye ule wa bio wa kutumia kilimo cha asili yaani bila ya matumizi ya madawa ya kemikali,hatua ambayo huchukuwa mwaka mzima. Kwa hivi sasa Nogamu inafanya kazi na wakulima wadogo wa bio milioni mbili lakini ni laki mbili tu ndio wenye vyeti ya kimataifa vya kusafrisha nje mazao yao. a

Siasa lazima ihitaji bio

' Suali hilo pia linamfikia mkuu wa chama cha wakulima wa bio : Kweli barani Afrika inawezekana kuongeza mapato hadi asilimia 80 kwa kilimo cha biolojia ? Kwa mujibu wa Muwanga anasema wao wameorodhesha kesi ambapo mapato ya mkulima yameongezeka maradufu baada ya kubadili kilimo na kuingia kile cha bio.Ardhi yake haiathiriwi na madawa ya kemikali na ndio maana kwa haraka inaleta tija lakini siasa haijatambuwa hilo kwa wakati unaotakiwa anakosoa Muwanga na kuemndelea kuisema kwamba" Bio manake pia ni uhifadhi hai wa mazingira,utaratibu huo wa kilimo asilia una vyakula zaidi na lishe ya kutosha, Mapato kwa wananchi yanazidi asilimia 80 na una nafasi kubwa kusafirishwa nje kwa bidhaa zake." Nchini Uganda usafirishaji nje wa mazao ya kilimo cha kawaida umekuwa ukipunguwa. Kwa miaka sita sasa muswada wa sheria juu ya kilimo endelevu cha bio umekuwa ukijadiliwa miongoni mwa wabunge.Muwanga anatumai pegine hatimae mwaka huu unaweza kupitishwa.

Wakati Moses Muwanga alipokuwa Ujerumani mwaka 2012 alitembelea Maonyesho ya Bidhaa za Bio na kupatiwa oda zenye thamani ya dola miloni mia mbili.Lakini hadi sasa Uganda inaweza tu kupeleka bidhaa za bio za thamani ya dola milioni 40.

Mwandishi :Ludger Schadomsky/ Mohamed Dahman

Mhariri: Alakonya, Bruce