1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DELHI:Mtu mmoja ajeruhiwa kwenye mripuko wa tatu wa bomu India

23 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFB5

Mtu mmója amejeruhiwa katika mripuko wa tatu uliofanywa katika mji mkuu wa India Delhi.

Mripuko huio umetokea saa chache baada ya mashambulio mengine ya bomu kufanywa katika majumba mawili ya kuonyesha cinema ambapo mtu mmoja aliuwawa na wengine 50 kujeruhiwa.

Majumba hayo yalikuwa yakionyesha cinema ambazo viongozi wa madhehebu ya Sikh wanasema ni za kuchukukiza katika imani yao.

Cinema hizo zilikuwa zikiwaonyesha watu wakiingia katika hekalu za madhehebu ya Sikh wakiwa na viatu miguuni.

Hata hivyo hakuna kundi lolote linalodaiwa kuhusika na mashambulio hayo.