Dortmund dhidi ya Real, Bayern dhidi ya PSG
25 Agosti 2017Mabingwa watetezi Real Madrid watapambana na Borussia Dortmund na Tottenham Hotspur katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabingwa mara tano Barcelona wamepangwa na makamu bingwa wa msimu uliopita Juventus, pamoja na mabingwa wa Ugiriki Olympiakos na Sporting Lisbon.
Bayern Munich, watakuwa na kibarua dhidi ya Paris Saint Germain, pamoja na Celtic na Anderlecht. Timu nyingine pekee ya Ujerumani, RB Leipzig ambao wanacheza kwa mara yao ya kwanza katika Champions League, watachuana na Monaco, Porto na Besiktas ya Uturuki.
Wakati huo huo, mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji wa kwanza kushinda mara tatu tuzo ya UEFA ya mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya. Mreno huyo alimpiku nyota wa Barcelona Lionel Messi na mlinda mlango wa Juventus Gianluigi Buffon. Katika upande wa wanawake, tuzo hiyo ilimwendea kiungo wa Barcelona, Mholanzi Lieke Martens
Orodha ya Droo kamili:
Kundi A: Benfica, Manchester United, Basel, CSKA Moscow
Kundi B: Bayern Munich, Paris St-Germain, Anderlecht, Celtic
Kundi C: Chelsea, Atletico Madrid, Roma, Qarabag
Kundi D: Juventus, Barcelona, Olympiakos, Sporting
Kundi E: Spartak Moscow, Sevilla, Liverpool, Maribor
Kundi F: Shakhtar Donetsk, Manchester City, Napoli, Feyenoord
Kundi G: Monaco, Porto, Besiktas, RB Leipzig
Kundi H: Real Madrid, Borussia Dortmund, Tottenham, Apoel
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Josephat Charo