1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund uso kwa uso na Real

24 Oktoba 2012

Bayern ilipata ushindi mwembamba wa bao1-0 dhidi ya Lille ya Ufaransa,na mabingwa Chelsea kuangukia pua dhidi ya Shakhtar Donetsk,leo ni zamu ya ,Real Madrid na Borussia Dortmund, na Schalke 04 kuumana na Arsenal.

https://p.dw.com/p/16VnZ
Borussia Dortmund's Marco Reus (2nd R) celebrates his goal against Manchester City with team mates during their Champions League Group D soccer match in Manchester October 3, 2012. REUTERS/Phil Noble (BRITAIN - Tags: SPORT SOCCER)
kikosi cha Borussia DortmundPicha: Reuters

Shakhtar Donetsk ambayo haikupigiwa upatu kuizamisha Chelsea , mabingwa wa sasa wa Champions League, walifanya hivyo jana (23.10.2010) kwa ushindi wa mabao 2-1.

Kocha Roberto di Matteo ambaye kikosi chake kimepoteza mchezo wake wa kwanza tangu aliposhika wadhifa huo Machi mwaka huu , amesema kuwa Shakhtar ina rekodi nzuri inapocheza nyumbani, hususan dhidi ya timu za Uingereza. Ni vigumu sana iwapo unafungwa goli la haraka.

REFILE - CORRECTING TYPO IN NAME Chelsea's caretaker manager Roberto Di Matteo listens to a question during a news conference at his team's training ground in Cobham, southeast England May 15, 2012. REUTERS/Dylan Martinez (BRITAIN - Tags: SPORT SOCCER)
Kocha wa Chelsea Roberto Di MatteoPicha: Reuters

Ni aibu kwamba tumeweza kurejea katika mchezo wetu wakati muda umekwisha, ameongeza Di Matteo.

Matokeo hayo yameipa nafasi timu hiyo ya Ukraine kuchpa hadi nafasi ya kwanza katika msimamo wa kundi hilo la E, ikiwa na points saba, tatu zaidi ya Chelsea. Juventus ina points tatu na Nordsjaelland ina point moja.

Barcelona yaokoka dakika za mwisho

Barcelona inaongoza katika kundi G ikiwa na points tisa kutokana na ushindi mara tatu, mbele ya Celtic ambayo ina points nne wakati Spartak Moscow imesogea na kufikia points tatu baada ya kupata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Benfica.

FC Barcelona players celebrate their victory over Celtic during a Champions League soccer match group G at the Camp Nou in Barcelona, Spain, Tuesday, Oct. 23, 2012. (Foto:Manu Fernandez/AP/dapd).
Barcelona wakishangiria bao dhidi ya CelticPicha: AP

Manchester United ilitoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 3-2 baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya Braga.

Ni ushindi wa tatu wa Manchester na inashikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa na points tisa katika kundi H.

Real husumbuliwa na timu za Ujerumani

Leo ni zamu ya makundi A, B , C na D, ambapo Real Madrid ina miadi na mabingwa wa ujerumani Borussia Dortmund. Kocha wa vigogo hao wa soka nchini Uhispania na Ulaya , Jose Mourinho amesema kuwa timu hiyo inapaswa kufuta rekodi yao mbaya dhidi ya timu za Ujerumani wakati watakapoingia uwanjani leo mjini Dortmund.

Tuna tatizo la historia tukicheza katika ardhi ya Ujerumani, tumepata ushindi mara moja tu , ni michezo migumu dhidi ya timu ngumu, amesema Mourinho mwenye umri wa miaka 49.

Real Madrid's coach Jose Mourinho waits for the start of their Spanish King's Cup quarter-final second leg "El Clasico" soccer match against Barcelona at Nou Camp stadium in Barcelona January 25, 2012. REUTERS/Albert Gea (SPAIN - Tags: SPORT SOCCER HEADSHOT)
Kocha wa Real Jose MourinhoPicha: REUTERS

Licha ya kulinyakua mara tisa kombe la Ulaya , Real ina rekodi mbaya ikikumbana na timu za Ujerumani na katika michezo yake 23 nchini Ujerumani imepoteza mara 16 na ushindi wao pekee ulikuwa miaka 12 iliyopita.

Ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bayer Levekusen Septemba 2000 ni ushindi pekee wa Real nchini Ujerumani, lakini Dortmund inakabiliwa na kibarua kigumu kuizuwia Real baada ya Wahispania hao kuikandanika Ajax mabao 4-1 mjini Amterdam wiki tatu zilizopita.

Arsenal's manager Arsene Wenger reacts as he watches his team play against Queens Park Rangers during their English Premier League soccer match at Emirates Stadium, London, Saturday, Dec. 31, 2011. (AP Photo/Sang Tan)
Kocha wa Arsenal London Arsene Wenger,Picha: AP

Michezo mingine ni kati ya Ajax Amsterdam inakumbana na Manchester City katika kundi D. Porto inamiadi na Dynamo Kiev, Dinamo Zagreb inakabiliana na Paris St Germain katika kundi A, wakati Arsenal London inaikaribisha Schalke 04, Montpellier inaonyeshana kazi na Olympiakos piraeus, katika kundi B. Zenit St Petersburg inaikaribisha nyumbani Anderlecht ya Ubelgiji na Malaga iko nyumbani ikipimana ubavu na AC Milan.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri.Hamidou Oummilkheir