Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas, amesema wamefanikiwa kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona UVIKO ama COVID-19. Katika mahojiano na mwandishi wa DW mjini Dodoma Deo Makomba, Dr. Abbas amedai kuwa Tanzania kama ilivyo mataifa mengine ilichukua mtizamo tofauti katika hatua za kukabiliana na ugonjwa huo na kwamba Watanzania waendelee kuchukua tahadhari.