Kundi la waasi wa ADF limeendelea kufanya mashambulizi katika mji wa Beni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo watu wanane wameuawa wakati wanafunzi wakifanya maandamano kutaka amani katika eneo hilo. Isaac Gamba amezungumza na mbunge wa eneo hilo Mayombo Omari Fikiri kutaka kujua ni kwanini jeshi la Kongo limeshindwa kulidhibiti kundi hilo hadi sasa licha ya kuwa ni kundi dogo la waasi.