DRC katika jukwaa la mitindo
New York, Paris, Berlin-Kinshasa! Mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo unataka kuwa sehemu ya jukwaa la mitindo ya Kimataifa, wanamitindo wa nchi hiyo wanaonyesha ustadi wao katika wiki ya mitindo mjini humo.
Rangi za kuvutia
Wabunifu wa mitindo Congo wanapenda min'garo na madoido mengi. Ni muda mrefu tangu mitindo kama hii iandaliwe mjini Kinshasa, sasa mji huo unataka kujulikana kimataifa. Mitindo ya Kadi Kabala katika wiki ya mitindo ya Kinshasa mwaka 2015 ni ya kuvutia na kujiamini- inayoelezea nguvu za wanawake.
Mfano wa kuvutia Mali
Tambwe za Kazadi de Sikasso alipata msukumo wa kazi yake kutoka nchi nyengine za Afrika kwa mfano mitindo na tamaduni za watu wa kabila la Bambara-Kusini Mashariki mwa Mali na Maasai wanaopatikana nchini Kenya na Tanzania. Mbunifu huyo wa mitindo anatokea mkoa wa Katanga, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Sanaa kutoka mkoa wa Shaba
Sikasso anaishi na kufanya kazi mjini Lubumbashi, mji mkuu wa mkoa wa Kusini Mashariki wa Katanga unaojulikana pia kama mji wa “shaba nyekundu,” kwasababu ya madini mengi yalioko huko. Hata hivyo utajiri huo wa mali ghafi mara kwa mara husababisha migogoro ya umuagaji damu.
Mitindo ya Haute Couture nyumbani
Mbunifu wa mitindo Jose Esam anajulikana sana barani Ulaya kuliko Afrika. Anaishi mjini Paris na huko anatengeneza mitindo ya hali ya juu ya Haute Couture – kwa wanawake na wanaume. Kwa mara ya kwanza ameonyesha mitindo yake nchini mwake Congo.
Mitindo ya Kijasiri
Vya rahisi si bunifu. "Mitindo yangu ni ya adimu na ya kuvutia kwaajili ya wanawake watendaji na kwa matukio yoyote yale," anasema Jose Esam. Pia anatengeneza mapambo na kofia anazouza katika duka lake mjini Paris.
Mitindo ya Ghali
Betu Tshongo or "Kumeso" anajiweka katika mitindo ya kisasa, inayokukumbushia mitindo ya kifahari kama Gucci, Prada na mingine, akitumia rangi za utamaduni wa Afrika. Pia anatengeneza mikoba na viatu vya hali ya juu.
Kwa wanaume jasiri
Rangi za kuwaka na kuvutia ndio mitindo ya Straton Nondo. Vitambaa vizuri vinavyoenea mwilini, michoro ya kiafrika- Hapa utamaduni unachanganywa na mitindo ya kisasa. Kitu muhimu ni muonekano. Baadhi ya mitindo ya Straton Nondo inaelezea mitindo ambayo kwa sasa inawafuasi wengi katika nchi kadhaa za kiafrika.
Mtindo wa Dandy
Suti hizi kwa mfano, zifanana na mtindo wa "Sapeurs", kutoka Ufaransa ambazo wanaume wa Kicongo huvalia na kijivinjari katika maeneo ya mabanda ya Kinshasa . Wengi wanajinyima kula ili wavae nguo za mitindo ya aina hii. Zamani watu wengi waliigiza utanashati wa Kifaransa, lakini sasa imekuja na sura mpya ya kiafrika.
Mitindo iliyotengenezwa upya
Vuguvugu la Sapeurs-lilitoa ujumbe fulani katika wiki hiyo ya mitindo: Papa Griffe, moja wa wawakilishi wa mitindo ya kung'aa hakuonekana amevalia mtindo wa Dandy, badala yake alivalia nguo zilizotenenezwa kwa makaratasi, je ni muamko wa mazingira kwa watu wa Congo? Au ni kukataa mitindo ya kisasa?