1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yashuku watu 600 wameambukizwa kirusi cha corona

16 Machi 2020

Wizara ya afya nchini Kongo inasema takribani watu 600 wanashukiwa kuwa wameambukizwa virusi vya corona kutokana na watu hao kuwa na ushirikiano wa karibu na watu walioambukizwa na wagojwa watatu waliothibika.

https://p.dw.com/p/3ZX1L
Afrika Coronavirus Pandemie / Kenia
Picha: Reuters/B. Ratner

Baada ya mgonjwa wa tatu kuthibitishwa kuwa ameambukizwa na virusi vya corona katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, serikali ya nchi hiyo imeamua kuweka mkazo kwenye uhamasishaji dhidi ya kuenea kwa maambukizi  mapya.

Wizara ya afya ya nchi hiyo inashuku kuwa takribani watu 600 wameambukizwa virusi vya corona kutokana na watu hao kuwa na ushirikiano wa karibu na watu walioambukizwa na ndiyo maana ni muhimu kwa serikali kuwahimiza raia wachukuwe hatua za kujikinga. 

Siku ya Jumamosi serikali iliripoti kwamba mgojwa mwengine amethibitishwa kuwa na virusi hivyo. Mtu huyo alikuwa ametoka likizoni nchini Uswisi na hivyo watu  waliowasili pamoja naye katika ndege wanahofiwa huenda wakawa wameambukizwa na hivyo wanafuatiliwa kwa karibu.

Serikali inatilia maanani katika kuwasaidia waathirika ili wasije kuwaambukiza jamaa zao na raia wengine. 

Serikali yaunda tume

Frankreich | Franzosen wählen trotz Coronavirus neue Stadt- und Gemeinderäte
Wafanyakazi wakisafisha Picha: picture-alliance/AP Photo/C. Ena

Wizara ya afya imeunda timu mbalimbali na kuzipeleka mitaani na vijijini kwa ajili ya kuzungumza na raia kwa lengo la kujaribu kuzuia kuenea maambukizi ya virusi hivyo, kwa mujibu wa kiongozi wa kamati ya uchunguzi wa maradhi, Dk. runa Abedi, ambaye pia ni mratibu wa mapambano dhidi ya virusi vya korona.

Serikali ya Kongo imetoa ilani kwa wasafiri wanaowasili kuheshimu masharti mbalimbali yakiwemo ya kupimwa na kutoa taarifa zinazohusika na safari zao.

Msafiri atakayeonekana na dalili ya kuambukizwa virusi vya corona, yaani homa na kikohozi, atawekwa karantini na kupewa matibabu na "yule asiye na dalili ila ametokea katika moja wapo ya nchi zilizokumbwa na maambukizi ya virusi hivyo anatakiwa ajiweke karantini kwa hiari na kisha atafwatiliwa na wataalamu kutoka wizara ya afya," kwa mujibu wa Dk. Abedi.

Hofu imetanda nchini Kongo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona, wanachokiomba kwa serikali ni kujaribu liwezekanalo ili ugonjwa huo usije ukaeneya kwenye maeneo mengi ya nchi kama ulivyokuwa ugonjwa wa Ebola ambao uliangamiza maelfu mashariki mwa nchi hiyo.

Jean Noel Ba-Mweze, DW Kinshasa