1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droo ya makundi ya Europa League yafanyika

29 Agosti 2014

Timu za Ujerumani Wolfsburg na Mönchengladbach zimepokea wapinzani wao katika hatua ya makundi ya Europa League. Gladbach itataraji kufuzu kwa urahisi wakati Wolfsburg wakipewa wapinzani wagumu

https://p.dw.com/p/1D3pr
Auslosung Europa League
Picha: Harold Cunningham/Getty Images

Borussia Mönchengladbach imepangwa katika kundi linaloonekana kuwa rahisi katika safari yake ya kutafuta ubingwa wa Europa League. Klabu hiyo ya Ujerumani itachuana na Villareal ya Uhispania, FC Zürich ya Uswisi na Apollon Limassol ya Cyprus.

Wolfsburg wka upande wao wamepewa kundi gumu, huku wakitarajiwa kupambana na Lille, Everton, na klabu ya Urusi ya Krasnador. Everton ilimaliza katika nafasi ya tano kwenye Ligi ya Premier ya English msimu uliopita nayo Lille ni mshirika wa kila mara katika Champions League.

Duru ya kwanza ya mechi za makundi za Europa League itachezwa Septemba 18, siku mbili baada ya mechi za kwanza za makundi katika Champions League.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu