1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI : Leo ni Ramadhan kwa baadhi ya nchi

23 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9u

Saudi Arabia mahala kulikozaliwa Uislamu itaanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan leo hii pamoja na mataifa kadhaa ya Ghuba.

Mabaraza makuu ya kidini nchini Saudi Arabia,Bahrain, Kuwait,Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu yamesema mwezi umeonekana baada ya magharibi na kuashiria kuanza kwa Ramadhan,

Misri ambalo ni taifa lenye idadi kubwa ya watu katika ulimwengu wa Kiarabu na Oman zimesema zitaanza kufunga hapo kesho.Mapema Libya ilitangaza kwamba Ramadhan ingelianza leo hii na shirika la habari la serikali lilimkariri kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi akidokeza kwamba Waislamu wanapaswa kufuata nyayo za Uislamu sahihi kutoka Libya.

Wakati wa kuanza kwa Ramadhan ambapo waumini wa dini ya Kiislam hufunga kwa kujizuwiya kula na kunywa na kila aina ya maasi kuanzia alfajiri hadi jua linapotua kunaweza kukatofautiana katika nchi tafauti za Kiislam duniani kwa kutegemea kuonekana kwa mwezi.