DUBAI: Osama Bin Laden kutoa ujumbe mpya
7 Septemba 2007Matangazo
Kiongozi wa Al-Qaeda,Osama Bin Laden anatazamia kutoa ujumbe mpya kwenye kanda ya video kuadhimisha miaka sita tangu kufanywa mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001.Tangazo hilo limetolewa na tovuti ya wanamgambo wa Kiislamu Al-Sahab,ambayo pia imeonyesha picha ya Bin-Laden kutoka kanda hiyo ya video.Ujumbe wa mwisho wa Bin Laden kwenye kaseti ya video, ulitolewa mwaka 2004.