Enerlid Franca, Sâo Tomé na Principe
23 Mei 2013Matangazo
"Umoja wa Afrika kwangu mie ni mradi ambao haukufaulu. Ingebidi watu wafanye kama katika Umoja wa Ulaya: Katika kipindi cha miaka 20 tu iliyopita Umoja wa Ulaya umefanikiwa kufanya mengi zaidi kuliko yale yaliyofikiwa katika miaka 50 ya Umoja wa Afrika tunayoisherehekea hivi sasa. Kuna tofauti kubwa kati ya jumuia hizo mbili. Kati ya wanachama wa Umoja wa Afrika hakuna ushirikiano hata kidogo katika masuala ya kiuchumi."