SiasaAsia
Erdogan aahidi kukabidhi madaraka iwapo atashindwa uchaguzi
13 Mei 2023Matangazo
Akizungumza Ijumaa usiku katika televisheni, Erdogan amesema nchini Uturuki wanaingia madarakani kwa njia ya kidemokrasia, na iwapo nchi hiyo itaamua tofauti, atafanya kile ambacho demokrasia inahitaji.
Alikuwa akijibu swali aliloulizwa kama atang'ang'ania madaraka. Amefafanua kuwa chama chake kitaheshimu matokeo yoyote yatakayotoka katika sanduku la kura.
Rais huyo wa Uturuki amesema kama upinzani una wasiwasi kuhusu usalama wa uchaguzi, wanapaswa kufuatilia vituo vyote vya kupigia kura na kuhakikisha usalama, kama ambavyo chama chake kitafanya.
Hata hivyo, Erdogan amesema anaamini atachaguliwa tena kwa muhula mwingine, pamoja na kupata wabunge wengi katika uchaguzi wa kesho.