Eritrea leo imefungua tena ubalozi wake nchini Ethiopia baada ya wiki iliyopita kumaliza miongo miwili ya mkwamo wa kijeshi kutokana na vita vya mpaka. Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na rais wa Eritrea Isaias Afwerki walifungua ubalozi huo katika mji mkuu Addis Ababa, hatua inayoelezwa kuwa muhimu katika mchakato wa kujongeleana baina ya mataifa hayo. Sikiliza maohojiano yafuatayo.