1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eti Burkina faso itazusha maajabu katika kombe la mataifa barani Afrika?

30 Januari 2013

Macho ya mashabiki wa dimba barani Afrika yanakodolewa Nelspruit wanakopimana nguvu watoto wa Togo na Tunisia,kujua nani atachuana na Burkina faso katika robo fainali ya kombe la mataifa barani Afrika.

https://p.dw.com/p/17UYe
Kitambulisho cha michuano ya fainali ya komve la mataifa barani Afrika mwaka 2013Picha: Getty Images

Baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya kombea la mataifa barani Afrika,Burkina faso kwa mara ya kwanza ugenini,inaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kukiuka vizingiti vilivyosalia na kusonga mbele katika uwanja wa Mbombela na hata kwenda mbali zaidi.Ushahidi umepatikana watoto wa Burkina faso walipotoka sare bila ya kufungana na Zambia na kushikilia usukani wa kundi C.

Mbinu za Burkina faso ndizo zilizowafanya wamalize sare pia bila kwa bila na Nigeria na kuishinda Ethiopia manne kwa yai,huo ukiwa ushindi wake wa kwanza katika michuano ya kombe la mataifa barani Afrika tangu Burkina faso ilipoandaa michuano hiyo mwaka 1998.

Burkina faso itamenyana jumapili ijayo katika uwanja wa Mbombela na mshindi wa pambano la leo hii kati ya Togo na Tunsia .

"Hatujui tutapambana na nani,kwa hivyo tunasubiri.Tunajua lakini tutachezea Nelspruit-na huko ni bora kwetu."amesema kocha wa Burkina faso Paul Put anaeutaja uwanja huo kuwa ni "uwanja wao wa nyumbani."

Burkina faso yapigiwa upatu

Afrika Cup 23.01.2013
Mashabiki wa Afrika kusini washangiriaPicha: Reuters

Itafaa kusema hapa kwamba wanasoka sita kati ya 23 wa timu ya taifa ya Burkina faso wanachezea katika timu za divisheni ya kwanza za Ufaransa,wanne tu wanachezea vilabu barani Afrika.

"Kila kitu kinawezekana kwasababu Burkina Faso wana wachezaji katika nchi za Ulaya,wamekuwa wakishiriki mara nyingi katika michuano ya kombe la mataifa barani Afrika bila ya kufanikiwa kuingia robo fainali" amesema mchezaji wa kati wa Zambia Rainford Kalaba aliyeongeza tunanukuu:"Hii ni fursa kwao kuaonyesha mashabiki wao nyumbani kile wanachoweza kukifanya kwa nchi yao."Mwisho wa kumnukuu Rainforf Kalaba wa Zambia.

Wakati huo huo mshambuliaji wa Burkina faso Alain Traoré,mwanasoka aliyepachika magoli mengi zaidi katika michuano hii ya kombe la mataifa barani Afrika hadi sasa,ameshayaaga mashindano hayo kutokana na kuumia paja la kushoto katika pambano la jana dhidi ya Zambia.

Wanariaadha wa kenya wachunguzwa

London 2012 - Leichtathletik
David Lekuta Rushida wa Kenya akishangiria ushindi wa mbio za mita 800 katika michezo ya Olympic ya London mwaka 2012Picha: picture-alliance/dpa

Tumalizie ukurasa wetu wa spoti kwa ripoti kutoka Kenya:wanariadha 32  wameridhia kutolewa damu ili ifanyiwe uchunguzi na kumaliza dhana dhidi yao .Habari hizo zimetangazwa na mwenyekiti wa shirikisho la wanariadha wa Kenya Isaiah Kiplagat .

Mandishi:Hamidou Oummilkheir/AP(AFP

Mhariri:Yusuf Saumu