Zaidi ya watu milioni mbili Kenya wanatatizwa na funza na milioni kumi wapo katika hatari ya kuvamiwa na funza. Tatizo hilo la funza ni baya mno hadi serikali kutangaza kuwa tarehe 3 mwezi Machi kila mwaka, ni siku ya kupambana na funza na kuhamasisha umma kuhusu jinsi ya kukabiliana nao.