1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fayulu kuwasilisha pingamizi dhidi ya matokeo ya uchaguzi

Sekione Kitojo
12 Januari 2019

Mshindi  wa  pili  katika  uchaguzi  katika  Jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya Congo  Martin Fayulu ametangaza  jana  Ijumaa  kuwa  atawasilisha pingamizi  mahakamani  dhidi  ya  matokeo  ya  uchaguzi  wa  rais

https://p.dw.com/p/3BQou
DR Kongo Wahlen Kandidat Martin Fayulu
Picha: Reuters/B. Ratner

Wakati  huo  huo , wakati muungano  wake  wa  upinzani  umesisitiza  kwamba  alipata  asilimia  61 ya kura  kwa  mujibu wa  uchunguzi wa  waangalizi  wa  kanisa  katoliki  lenye  ushawishi mkubwa .

Fayulu  alizungumza  na  mamia  kwa  maelfu  ya  waungaji  wake  mkono ambao  walikusanyika  katika  mji  mkuu  Kinshasa, kupinga  kile  walichokiita "ushindi  wa  wananchi  ulioibiwa."

DR Kongo nach Wahlen Martin Fayulu Anhänger
Martin Fayulu mgombea wa upinzani nchini CongoPicha: Reuters/B. Ratner

Polisi  wengi  walionekana wakishika  doria  katika  mji  huo  mkuu. Mfanyabiashara  na mwanaharakati  anayefanya  kampeni  dhidi  ya  rushwa iliyokithiri  nchini  Congo, Fayulu  amemshutumu  rais  anayeondoka madarakani  Joseph Kabila  kwa  kufanya  makubaliano  ya  chini kwa  chini na  mshindi  aliyetangazwa , kiongozi  wa  upinzani  ambaye  hajajihusisha sana  na  siasa  Felix Tshisekedi.

Kanisa  katoliki , mamlaka  adimu  ambayo  Wakongo  wengi  wanaliamini, limesema  wachunguzi  wake  40,000  wa  uchaguzi  wamempata  mshindi tofauti kutoka  matokeo rasmi  lakini  halikutoa  maelezo  zaidi.

Uchunguzi  wa  kanisa  hilo  umegundua  Tshisekedi  alipata  asilimia  18  ya kura , juu  kidogo  ya  mgombea  wa  chama  tawala  Emmanuel  Ramazani Shadary, muungano  wa  Fayulu  umesisitiza.

Demokratische Republik Kongo | Emmanuel Ramazani Shadary, Präsidentschaftskandidat in Kinshasa
Mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani ShadaryPicha: Getty Images/AFP/J. Wessels

Matokeo yachapishwe

Fayulu  ametoa  wito  kwamba tume  ya  uchaguzi  ya  Congo  ichapishe maelezo  ya  matokeo, kituo  kwa  kituo, na  kusema  atawasilisha  mashauri mahakamani  leo  Jumamosi asubuhi (12.01.2019) kupinga  matokeo  hayo. Aliwatupia  busu watu  waliokusanyika. "Wale  ambao  wamekuwa  wajinga kuchapisha  matokeo  bandia, tutapambana  nao," alisema.

Wacongo  wanakabiliwa  na  hali isiyokuwa  ya  kawaida  ya  uchaguzi unaodaiwa  kuwa  umechakachuliwa  kuelekea  upinzani  baada  ya mgombea  aliyependelewa  na  Kabila , Shadary , kufanya  vibaya  katika uchaguzi.

DR Kongo Politiker Felix Tshisekedi
Mshindi wa uchaguzi wa Congo aliyetangazwa na tume ya uchaguzi CENI Felix TshisekediPicha: Getty Images/AFP/V. lefour

Tume  ya  uchaguzi  mapema  siku  ya  Alhamis  ilitangaza   kwamba Tshisekedi  alishinda  kwa  asilimia  38  ya  kura  wakati  Fayulu  alipata asilimia  34.

"Mabadiliko  hayawezi  kujadiliwa  nyuma  ya  pazia  na  madaraka  yanakuja tu  kutokana  na  sanduku  la  kura, hakuna  njia  nyingine," amesema muungaji  mkono  wa  Fayulu  Jean Otaba , mwenye  umri  wa  miaka  28. "Unaweza  kuona  hakuna  sherehe  kubwa  licha  ya  tangazo  hilo. Hii  ni kwasababu  sio  kweli.

Kongo Joseph Kabila
Rais anayeondoka madarakani Joseph KabilaPicha: picture alliance/AP Photo/J. Bompengo

wakati  huo  huo vyama  vinavyomuunga  mkono  rais  anayeondoka madarakani  nchini  Congo Joseph Kabila  vimeshinda  wingi  katika uchaguzi  uliocheleweshwa  wa  bunge, kwa  mujibu  wa  ukusanyaji  wa hesabu  uliofanywa  na  shirika  la  habari  la  AFP leo.

Vyama  vinavyomuunga  mkono  Kabila  vimevuka  kiwango  cha  viti  250 kinachotakiwa  kuwa  na  wingi  bungeni  katika  bunge  la  taifa lenye  viti 500, kwa  mujibu  wa  matokeo yaliyowekwa  pamoja  na  tume  huru  ya  taifa  ya uchaguzi  CENI.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape