Gabon yaaga mashindano ya Afcon
23 Januari 2017
Huko mjini Libreville ambako timu 16 za mataifa ya Afrika zinawania ubingwa wa mataifa hayo katika kombe la Afrika , ambapo jana Jumapili kundi A lilimaliza michezo yake na wenyeji wa mashindano Gabon kuaga mashindano hayo baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Simba wa nyika Cameroon.
Guinea Bissau ilikubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso na hivyo Burkina Faso kutinga katika robo fainali pamoja na Cameroon.
Jumatatu kutakuwa na mpambano kati ya Zimbabwe ikipambana na Tunisia wakati huo huo Senegal ikipambana na Algeria.
Kuna hali ya wasi wasi mkubwa kuhusiana na ubora wa viwanja katika mashindano haya ya Afcon. Hali hii inaelezwa kuwa imechangia kuzorotesha ubora wa michezo hiyo na ukame wa mabao pia huku wachezaji hasa wanaocheza soka ya kulipwa katika mataifa ya Ulaya wakicheza kwa tahadhari kubwa.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / dpae / rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahhman