SiasaUrusi
The Moscow Times yaorodheshwa kama wakala wa kigeni
18 Novemba 2023Matangazo
Wizara ya sheria ya Urusi jana ililiongeza gazeti la mtandaoni la The Moscow Times lenye umaarufu miongoni mwa jamii ya wataalamu wa Urusi kwenye orodha yake ya mawakala wa kigeni. Hatua hiyo ni muendelezo wa msako mkali unaoendeshwa na serikali ya nchi hiyo dhidi ya vyombo vya habari vinavyoikosoa pamoja na vyama vya upinzani.
Athari ya kuorodheshwa kama wakala wa kigeni
Jina la mawakala wa kigeni, huwaweka watu binafsi na mashirika chini ya uchunguzi mkali wa kifedha na huhitaji taarifa zao zijumuishe notisi ya kueleza kuwa wametajwa kuwa mawakala wa kigeni.
Kutajwa kwa watu binafsi na mashirika kuwa mawakala wa kigeni, kunaonekana kama udhalilishaji unaolenga kuhujumu uadilifu wa walioorodheshwa.