GENEVA : Chama cha sera za kizalendo chashinda uchaguzi
22 Oktoba 2007Matangazo
Chama cha Utaifa cha Wananchi wa Swirtzerland cha msimamo mkali wa mrengo wa kulia kimejisombea asilimia 29 ya kura katika uchaguzi wa bunge la taifa baada ya kampeni kali ambayo imewalaumu wageni kwa kuhusika kwa kiasi kikubwa na uhalifu nchini humo.
Matokeo rasmi yaliyotolewa leo hii na Ofisi ya Takwimu yameonyesha kwamba chama hicho cha SVP kimepita kile cha kutetea biashara cha Radical Demokrat kilichopata asilimia 28 ya kura wakati ulipoitishwa uchaguzi mpya wa Swirtzerland mara baada ya Vita Kikuu vya Kwanza vya Dunia.
Chama cha mrengo wa shoto cha Kijani kimejiimarishan kidogo kwa kupata asilimia 9.6 ya kura kutoka asilimia 7.9 iliyopata miaka minne iliopita.
Chama cha Kisoshalisti kimepata pigo kubwa.