GENEVA: Raia wazidi kuyatoroka machafuko nchini Irak
13 Oktoba 2006Matangazo
Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, limesema watu 40,000 huikimbia Irak kila mwezi na wengine zaidi ya milioni1,5 walilazimika kuyahama maskani yao na kuwa wakimbizi wa ndani. Msemaji wa Shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR, amesema maelfu ya makumi ya raia wa Irak wamekimbilia katika nchi za Uturuki, Lebanon, Misri, nchi za Huba na Ulaya. Amesema sababu zinazopelekea raia hao kuitoroka Irak ni machafuko ya kidini na mauaji yanayoendelea kuisibu nchi hiyo.