1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guardiola aipeleka Man City fainali ya Ligi ya Mabingwa

6 Mei 2021

Baada ya muongo mmoja wa kukatishwa tamaa, Pep Guardiola amerejea katika fainali ya Ligi ya Mabingwa na amebaki na mechi moja tu akitimiza jukumu lake la kuwafanya Man City kuwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza

https://p.dw.com/p/3syJ9
Champions League Halbfinale - Manchester City v Paris St Germain
Picha: Paul Ellis/AFP/Getty Images

Katika mpambano kati ya vilabu viwili tajiri lakini ambavyo havijawahi kushinda Ligi ya Mabingwa, Man City ilionyesha kandanda safi na kuichapa Paris Saint-Germain jumla ya mabao 4-1 katika mikondo miwili ya nusu fainali.

Riyad Mahrez, alifunga mabao mawili katika ushindi wa 2 - 0 wa mkondo wa pili wa nusu fainali jana usiku, huku Angel di Maria wa PSG akionyeshwa kadi nyekundu. City watacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia yao, dhidi ya Real Madrid au Chelsea mjini Instabul. Chelsea inawaalika leo usiku Real Madrid mjini London.