1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guardiola kuondoka Bayern mwakani

21 Desemba 2015

Suala lingine linalogonga vichwa vya habari wiki hii ni uamuzi wa kocha nyota wa Bayern Munich kuitupa mkono timu hiyo , baada ya mkataba wake kumalizika katikati ya mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/1HRHJ
Bundesliga 17. Spieltag Hannover 96 - FC Bayern München
Picha: Getty Images/Bongarts/S. Franklin

Uamuzi wa Pep Guardiola kuachana na timu hiyo Juni mwakani umezusha wimbi la uvumi nchini Uingereza kuhusu wapi atakakotua. Mhispania huyo anahusishwa na timu ya Manchester City , Chelsea na Manchester United.

Uamuzi wa Pep kuitelekeza Bayern ulitangazwa jana Jumapili na klabu yake hiyo ya Bayern .

Pep Guardiola ameshinda mataji matano katika klabu hiyo tangu mwaka 2013 na anawania mataji mengine matatu msimu huu.

Pamoja na mafanikio yake katika Barcelona kuanzia mwaka 2008 hadi 2012 ni hakika kwamba Guardiola atakuwa ni kocha anayesakwa mno na vilabu itakapofika mwezi Julai mwakani.

Fußball Carlo Ancelotti Trainer Paris Saint-Germain
Picha: Getty Images/AFP

Kituo chake kinachoonekana wazi kitakuwa katika Premier League, ambako anahusishwa na vigogo kama Manchester City, Chelsea na Manchester United.

Kocha wa City manuel Pellegrini anahisi kwamba ni suala tu la wakati kabla ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 kutua Uingereza.

Guardiola anaonekana na wachunguzi wa masuala ya soka kuwa atafanyakazi na Manchester City msimu ujao licha ya kwamba Pellegrini , ambaye ameshinda ubingwa wa ligi ya Uingereza mara mbili, ana mkataba hadi mwaka 2017.

Kocha wa Arsenal London Arsene Wenger amesema ongezeko la fedha zinazopatikana kwa michezo ya soka kuoneshwa katika televisheni zimezifanya timu ndogo kuwavutia wachezaji wazuri kutoka Ulaya na kuifanya ligi hiyo ya Uingereza kuwa na ushindani mkubwa. Kitu cha wazi ni kwamba Premier League ina uwezo mkubwa sana kifedha ambapo timu za chini ambazo matumizi yake ni madogo, bado zinaweza kununua wachezaji bora kutoka Valencia, Lyon, na hii inaifanya ligi hii kuwa na ushindani zaidi, Wenger amesema kabla ya pambano la leo kati ya Arsenal London dhidi ya Manchester City.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman