Guterres kufanya ziara mpakani mwa Misri na Gaza leo
23 Machi 2024Matangazo
Safari ya Guterres inafanyika katika wakati ambapo Israel inatishia kufanya operesheni kubwa ya kijeshi katika mji wa Rafah ulioko kwenye mpaka huo na Misri, licha ya miito ya kimataifa inayoitaka nchi hiyo iachane na mpango huo.
Takriban wakaazi milioni 2.3 wa Gaza wanajihifadhi katika eneo la Rafah, ingawa hali ya kiutu inatajwa kuzorota zaidi katika upande huo wa Kaskazini mwa Gaza huku mzozo ukiendelea.
Soma pia:Netanyahu: Israel itaendelea na mpango wa kuishambulia Rafah
Mbali ya mpaka huo, Katibu Mkuu huyo pia atakitembelea kitongoji cha Al Arish kaskazini mwa rasi ya Sinai nchini Misri, ambako misaada mingi ya kimataifa inahifadhiwa kabla ya kupelekwa Ukanda wa Gaza.