Hagari aomba radhi kwa kukosoa mswada juu ya uvujaji siri
5 Desemba 2024Katika mkutano na waandishi wa habari, Hagari amesema marekebisho ya kisheria yaliyozingatiwa na wabunge yalikuwa hatari kwa jeshi na usalama wa nchi hiyo.
Hagari alikosolewa kwa haraka na mkuu wa jeshi la Israel Herzi Halevi, na akaomba msamaha kupitia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Soma pia: Jeshi la Israel lamuokoa mateka kusini mwa Gaza
Hagari, alisema katika taarifa yake wakati wa kujibu maswali, alijieleza kwa namna iliyozidi mamlaka yake kama msemaji wa jeshi, na kusababisha shtuma hizo dhidi yake.
Hagari ameongeza kuwa taifa la Israel ni nchi huru na kwamba jeshi liko chini ya uongozi wa kisiasa.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amepongeza kukosolewa kwa Hagari, akisema kwamba katika nchi ya kidemokrasia, jeshi halipaswi kuingilia kati masuala ya kisiasa na kukosoa sheria.