Cheche za maneno zinaendelea kurushwa kati ya serikali ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuhusiana na suala la waasi wa M23 ambao serikali ya Kongo inasema wanaungwa mkono na Rwanda. Tatu Karema amezungumza na mwandishi wa DW Saleh Mwanamilongo ambaye ni mtaalam wa masuala ya Kongo na kanda ya Maziwa Makuu na hapa anaeleza kuhusiana na jinsi hali ilivyo Nyiragongo.