HANOI:Japan yaahirisha mazungumzo na Korea Kaskazini bila sababu
7 Machi 2007Matangazo
Korea Kaskazini imeahirisha mazungumzo kati yake na nchi ya Japan yaliyokubaliwa kufanyika ili kujaribu kusitisha mpango wake wa nuklia bila kutoa sababu yoyote au lini mazungumzo hayo yataendelea.
Hii ni mara ya kwanza mataifa hayo mawili yanafanya mazungumzo baada ya kipindi cha mwaka mmoja cha kutosemezana.
Japan inakataa kutimiza makubaliano yaliyofikiwa mwezi jana pamoja na Marekani,Uchina,Urusi na Korea Kusini yanayoahidi kuipa nchi hiyo msaada wa mafuta endapo itasitisha mpango wake wa nuklia.
Wajumbe wa pande zote mbili walikutana mjini Hanoi mapema hii leo lakini kubadilisha ratiba ya mkutano mchana.