Harar, mji mtakatifu wa Kiislamu nchini Ethiopia
Harar ni kitovu cha Uislamu nchini Ethiopia na ukitajwa kuwa mji wa nne mtakatifu kabisa wa Kiislamu. Mwandishi wa DW Maria Gerth-Niculescu anakuongoza kupitia mitaani na masoko yaliyofurika kwenye mji huu mtakatifu.
Harar Jugol, mji mkongwe wa Mashariki
Mji wa Harar unatajwa kuwa umeanzishwa na wahamiaji wa Kiarabu kati ya kati ya karne ya 10 na 13. Mji mkongwe au Harar Jugol, unaweza kufikiwa kupitia milango mitano ya zamani kabisa. Ni mji mkuu wa jimbo dogo zaidi nchini humo linalokaliwa na idadi kubwa ya kabila ya Oromos. Harar iliyoko mashariki mwa nchi, imetambulishwa kama urithi wa Dunia na UNESCO tangu 2006.
Ni eneo la Hijja kwa Waislamu
Jiji la Harar una misikiti 82 na mahekalu zaidi ya 100. Msikiti Mkuu wa Jami ni misikiti mkubwa zaidi kwenye jiji hilo. Karibu theluthi moja ya Waethiopia ni Waislam - lakini hapa, wanajihesabu kuwa na idadi kubwa zaidi.
Msikiti kwa ajili ya wanawake
Msikiti wa Jami ni pekee ambapo wanawake wanaruhusiwa kuswali katika jengo moja kama wanaume. Wanaingia kupitia mlango huu mdogo upande wa kulia wa, lakini pia ni kawaida kuwaona wakiswali nje. Misikiti mingi katika mji huu wa kale ni midogo sana, na hivyo iko maalumu kwa ajili ya wanaume.
Mji wa amani
Kuna makanisa mawili ndani ya mji huo, kanisa la Medhane Alem ni la pekee la Orthodox. Wakazi wa Harar wanajivunia kuwa mji wao unakaribisha dini zote. Mwaka 2003, jiji hilo lilipata Tuzo ya Amani ya UNESCO kufuatia ushirikiano wa amani wa makundi mengi ya kikabila na ya kidini. Katika miaka ya hivi karibuni, hata hivyo kumekuwa na mvutano juu ya masuala ya ardhi na uwakilishi wa kisiasa.
Utakatifu utokanao na miujiza
Kuna kitu cha ajabu sana kuhusu mji huu wa watu zaidi ya 120,000. Sababu moja ya muujiza huu ni ushawishi wa madhehebu ya Sufi ambayo ni tawi Uislamu na ambalo mahusiano na Mungu yanapatikana kupitia mila na tafakari. Moja ya mahali patakatifu zaidi katika jiji hili ni kaburi la Sheikh Abadir, ambaye ni mmoja wa waasisi wa mji. Hapa watu hukaa kwa msaaa kadhaa wakitafuna mirungi.
Jani maalumu
Wakati mirungi hapo awali ilitumika kwa madhumuni ya kiroho, sasa hutumiwa sana nchini Ethiopia. Eneo linalozunguka Harar linabakia kitovu cha matumizi yake lakini pia na biashara. Unachangia karibu asilimia 70 ya mapato yatokayo na kilimo katika eneo hilo na hutafunwa na wanaume wengi lakini pia wanawake. Jani hili hupunguza uchovu na hamu. Husababisha uraibu linapotafunwa mara kwa mara.
Ununuzi wa vitambaa vya nguo
Uchumi wa Harar pia umeongezeka kutokana na soko la kitambaa. Mtaa huu unaitwa "makina girgir" kutokana na sauti ya mashine za kushonea. Mara nyingi huwa na wanawake wengi kutoka maeneo ya vijijini. Hununua vitambaa vipya na kuwapa wanaume ambao huwashonea nguo mpya na nzuri ama vitambaa vya kufunika vichwa.
Kila siku ni siku ya gulio
Kuanzia mapema asubuhi, WaOromo kutoka maeneo ya jirani huja mjini hapo kuuza bidhaa zao. Mara nyingi hutembea kwa masaa kadhaa na punda wao ili kuufikia mji wa Harar. Mapato hununuliwa vitu vipya kama vile sufuria, nguo au nyama kwa ajili ya kaya zao. Harar inanufaika na masoko ya walanguzi, masoko ya Kiislamu, soko la vyakula, soko la viungo.
Biashara ya ngamia
Soko maarufu la ngamia hufanyika mara mbili kwa wiki karibu kilomita 40 (24.8 maili) kutoka Harar. Hadi ngamia 200 huuzwa katika asubuhi moja, kuanzia karibu € 500 ($ 565) kwa ngamia mmoja. Wafanyabiashara wa ngamia kwa kawaida huwa ni wachungaji wa KiSomali. Ngamia hutumika kwa shughuli za usafiri na chakula.