Bahari ya Mediterenia imekuwa kama kaburi la halaiki kwa wahamiaji wa Afrika ambao wanatafuta kuingia Ulaya katika harakati za kutafuta maisha bora. Baada ya kusafiri mwendo mrefu kutoka nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara wahamiaji hao wengi wao wakiwa ni vijana kutoka nchi za Afrika Magharibi, Eritrea na hata Djibouti huishia katika vituo Libya.