1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatimaye Kabila akubali kung'atuka madarakani

Sylvia Mwehozi
8 Agosti 2018

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametangaza Jumatano kwamba hatogombea katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

https://p.dw.com/p/32pk8
Kongo Joseph Kabila
Picha: picture alliance/AP Photo/J. Bompengo

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametangaza Jumatano kwamba hatogombea katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

Hatua hiyo ya Kabila inatuliza wasiwiwasi uliokuwepo miongoni mwa upinzani na Jumuiya za kimataifa kwamba angejaribu kuwania muhula mwingine na kusalia madarakani.

Msemaji wa serikali amesema waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Ramazani Shadary ambaye kwa sasa ni katibu mkuu wa chama tawala ndiye atakayepeperusha bendera ya chama chake cha kisiasa, mnamo ambapo Congo ikikabiliwa na uchaguzi wa kwanza wa amani na makabidhiano ya madaraka ya kidemokrasia katika historia ya nchi hiyo.

Tangazo hilo limekuja saa chache kabla ya muda wa mwisho wa wagombea kujisajili kukamilika. Shadary atakuwa mgombea wa muungano wa vyama ulioundwa hivi karibuni wa Common front for Congo.

Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2001, kisheria hawezi kuwania muhula mwingine baada ya muda wake kumalizika mwishoni mwa 2016. Uchaguzi umeahirishwa tangu wakati huo na kuchochea maandamano.

Mwandishi: Sylvia Mwehozi

Mhariri: Iddi Ssessanga