1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA: Hali ya afya ya rais Castro yaugubika mkutano

15 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDC9

Hali ya afya ya rais wa Cuba, Fidel Castro, imeugubika mkutano wa mataifa yasiyo na mafungamano yoyote hii leo.

Runinga ya kitaifa nchini Cuba ilimuonyesha rais Castro akisimama kidogo na kumsalimia rais wa Venezuela, Hugo Chavez hapo jana. Rais Chavez amesema rais Castro amepona na anatembea na kuimba.

Chavez pia amedai kwamba Marekani inataka kumzuia asihudhurie mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, kwa kuwakataza visa za kusafiria wajumbe wengi wa Venezuela watakaoandamana naye.

Wakati huo huo, rais wa Iran amefanya mazungumzo na viongozi wa nchi zinazoendelea katika mkutano huo wa Havana na kuutetea mpango wa nyuklia wa nchi yake.