1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA : India na Pakistan kuanza tena mazungumzo

17 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDBb

India na Pakistan zimesema kwamba zitaanza tena mazungumzo rasmi ya amani.

Tangazo hilo limetolewa na Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa pamoja na Rais Pervez Musharraf wa Pakistan pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote nchini Cuba.Mazungumzo hayo yatakuwa ya ngazi ya mawaziri.Viongozi hao walifikia ufumbuzi huo baada ya mazungumzo yao yaliolenga mzozo wa Kashmir.Huo ni mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili tokea kuzuka kwa miripuko ya mabomu yenye maafa mjini Mumbai hapo Julai 11.

Mapema Musharraf alielezea matumaini yake kwamba mkutano huo unaweza kupelekea usitishaji wa mapigano katika mpaka wa nchi hizo kwenye Milima ya Himalaya.