1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HELSINKI.Mawaziri wa nchi za umoja wa ulaya kujadiliana juu ya DRC na Kosovo

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6t

Mawaziri wa ulinzi wa nchi za Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana kwa siku mbili nchini Finland.

Katika mkutano wao mawaziri hao watajadili jukumu la umoja huo katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Kosovo.

Umoja wa Ulaya unakabiliwa na shinikizo la kuongeza muda wa wanajeshi wake katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baada ya kumalizika kwa uchaguzi na kuhesabiwa kura ifikapo Desemba mosi.

Kwa sasa kuna wanajeshi 1000 wa umoja wa ulaya wakiongozwa na jeshi la Ujerumani.

Wakati huo huo mpatanishi wa umoja wa mataifa wa jimbo la Kosovo Marti Ahtisaari anatarajiwa kuwahutubia mawaziri wa Umoja wa Ulaya juu ya hali ya baadaye ya Kosovo.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka, huku jimbo la Kosovo likitarajiwa kupata utawala utakaosimamiwa.