1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hollande aishutumu DRC

14 Oktoba 2012

Rais Francois Hollande ameishutumu serikali ya Kongo kwa kukiuka haki za binadamu,na kutoa wito wa kusitishwa kwa mzozo wa mashariki ya nchi hiyo wakati wa mkutano wa viongozi wa Francophonie Jumamosi(13.10.2012)

https://p.dw.com/p/16Phk
France's President Francois Hollande, seen in this video grab from French private TF1 television, speaks during a prime time news broadcast at their studios in Boulogne-Billancourt, near Paris, September 9, 2012. REUTERS/Hand Out (FRANCE - Tags: POLITICS) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Rais wa Ufaransa Frankreich FrancoisPicha: Reuters

Ni viongozi 15 tu wa shirikisho la mataifa yanayozungumza Kifaransa , Francophonie, lenye wanachama 75 wamehudhuria mkutano huo unaofanyika katika jengo la bunge mjini Kinshasa pamoja na mwenyeji wa mkutano huo , rais wa Kongo, Joseph Kabila. Hollande , ambaye ameikasirisha jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kwa kusema hali ya haki za binadamu nchini humo haikubaliki, amerudia tena usemi wake huo katika mazungumzo ya ana kwa ana na ya uwazi , pamoja na rais Kabila muda mfupi kabla ya mkutano huo kuanza.

Akizungumza baada ya mikutano mingine na wawakilishi wa upande wa upinzani na asasi zisizokuwa za kiserikali, Hollande amesema: "Francophonie sio tu lugha ya Kifaransa," na kuongeza kuwa "kuzungumza Kifaransa pia kuna maana ya kuzungumzia juu ya haki za binadamu, kwasababu haki ya mtu imeandikwa kwa Kifaransa, " akimaanisha mkataba wa umoja wa mataifa juu ya haki za binadamu, ulioandikwa na wanamapinduzi wa Kifaransa.Kiongozi huyo wa Ufaransa pia alikutana na kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi.

DR Congo elections epa03017273 Top opposition leader Etienne Tshisekedi (C) arrives for a news conference at his residence in Kinshasa, the Democratic Republic of Congo, 27 November 2011. The veteran politician vowed to hold a public rally, defying a government order banning political rallies after at least three people had reportedly been killed in a clash on previous day. Presidential and parliamentary elections are scheduled to be held in DR Congo on 28 November 2011 amid concerns over the prospects for fair elections. Tshisekedi, a 78-year-old opposition leader and the head of the Union for Democracy and Social Progress (UDPS), and Vital Kamerhe, a former UDPS member, are among many others who are challenging incumbent Joseph Kabila in the country's second election since the end of a bloody civil war in 2003. Election-related violence has already broken out in parts of the country ahead of the poll. Election official has said on 27 November that there will be no delay and elections will go as planned on 28 November, despite concerns by many that it would be delayed due to the violence and logistical difficulties in the country two-thirds the size of Western Europe. EPA/DAI KUROKAWA
Kiongozi wa upinzani DRC Etienne TshisekediPicha: picture-alliance/dpa

Mada muhimu mashariki ya DRC

Uasi wa matumizi wa nguvu na mizozo ya kikabila inayolikumba eneo la mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo inatarajiwa kuwa mada muhimu katika mkutano huo. Hali nchini Mali pia itakuwa mada muhimu, ambako wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali wamechukua udhibiti wa eneo la kaskazini mwa Mali.

Hollande amekanusha madai yaliyotolewa na kiongozi wa kundi moja la wapiganaji kuwa uungaji wake mkono wa kuingilia kati kijeshi dhidi ya Waislamu wenye itikadi kali wanaodhibiti eneo la kaskazini ya Mali , umeweka maisha ya raia wa Ufaransa waliotekwa nyara katika hatari. Oumar Ould Hamaha, kiongozi wa moja ya makundi ya waasi wenye mafungamano na kundi la al-Qaeda katika eneo la Maghreb (AQIM), amesema Hollande pia ameweka maisha yake binafsi katika hatari.

Maisha ya mateka hatarini

"Maisha ya mateka raia wa Ufaransa hivi sasa yamo katika hatari kwasababu ya matamshi ya rais wa ufaransa ambaye anataka kupigana vita dhidi yetu, " amesema Hamaha, kutoka kundi la harakati za umoja na jihad katika Afrika magharibi (MUJAO)."Maisha yake binafsi pia yamo hatarini. Anapaswa kufahamu hilo," aliongeza.

EXCLUSIVE IMAGES A still from a video shows armed Islamists patrolling in the streets of Gao on June 27, 2012. Algerian jihadists arrived in Gao on June 29, 2012 to reinforce Islamist fighters in the northern Mali city after they chased Tuareg rebels from the town they had jointly occupied for three months, sources said. The Islamist group which drove out the Tuareg in fighting that caused 20 deaths, the Movement for Oneness and Jihad in West Africa (MUJAO), along with AQIM and Ansar Dine (Defenders of Faith) have taken firm control of Mali's vast north. Ansar Dine leader Iyad Ag Ghaly arrived in the town on June 28, after the fighting a day earlier erupted between the Tuareg and Islamists resulted in the desert nomads being dislodged from all key positions in the city. AFP PHOTO (Photo credit should read STR/AFP/GettyImages)
Wapiganaji wa Kiislamu kaskazini mwa MaliPicha: AFP/Getty Images

AQIM kwa hivi sasa inawashikilia mateka tisa kutoka mataifa ya Ulaya katika eneo la Sahel, sita kati yao ni Wafaransa. Hollande amekanusha matamshi hayo, wakati akiwa mjini Kinshasa. "Ni kutokana na kuonyesha nia halisi katika kusisitiza sera zetu, ambazo ni kupambana na ugaidi, ambapo tunaweza kuwashawishi wateka nyara kwamba umefika wakati wa kuwaachia huru ," amewaambia waandishi habari.

Kabila alikaribishwa kwa shangwe kubwa wakati mkutano huo ukifunguliwa. Kwingineko mjini Kinshasa hata hivyo, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji kadha wanaoipinga serikali , ambao walikuwa wakitupa mawe na ambao walikaidi amri ya kutofanya maandamano. Wanadai kuwa kuchaguliwa tena kwa rais Kabila katika mwaka 2011 kulihusika mno na udanganyifu.

Newly arrived refugees from the Democratic Republic of Congo walk a sheep through a makeshift refugee camp at Bunagana near Kisoro town 521km (312 miles) southwest of Uganda capital Kampala, May 15, 2012. The refugees fled the Masisi region in Congo's North Kivu province since fighting broke out between Congolese troops and fighters loyal to a renegade general Bosco Ntaganda. Clashes erupted after Congolese President Joseph Kabila announced last month he would try to arrest renegade General Ntaganda, wanted by the International Criminal Court (ICC) for war crime in northeastern Congo's ethnic conflict. Picture taken May 15, 2012. REUTERS/James Akena (UGANDA - Tags: SOCIETY CIVIL UNREST POLITICS ANIMALS)
Watu waliokimbia makaazi yao ndani ya DRC kutokana na vita mashariki mwa nchi hiyoPicha: Reuters

Kabila amezungumzia kuhusu vita ambavyo ni kinyume na sheria , vinavyofanywa na watu kutoka nje katika eneo la mashariki ya nchi hiyo.

"Wakati watu wetu wanachukua juhudi zote kuendeleza maisha yao, makundi fulani yenye maslahi kutoka nje yamekuwa kwa miezi kadha yakifanyakazi kuidhoofisha nchi yetu katika jimbo la Kivu ya kaskazini, katika mpaka wa mashariki na Rwanda," Kabila amesema katika mkutano huo.

epa03029391 (FILE) A file picture dated 24 October 2011 shows Joseph Kabila, President of the Democratic Republic of Congo, looking on, during the closing news conference at the Francophone Summit in Montreux, Switzerland. Incumbent Joseph Kabila was on 09 December 2011 declared the winner of last month's presidential elections in the Democratic Republic of Congo, defeating 10 other candidates, according to the country's election commission. The results still need to be confirmed by the supreme court. According to media reports on 09 December 2011, opposition leader Etienne Tshisekedi has declared himself president, only a few hours after hours after provisional results shows that Joseph Kabila had won. EPA/DOMINIC FAVRE *** Local Caption *** 00000402410042
Rais Joseph KabilaPicha: picture-alliance/dpa

Hakuitaja Rwanda kwa jina , nchi ambayo imeshutumiwa kwa kuwaunga mkono waasi katika eneo hilo, dai ambalo lilisababisha kuletwa kwa wachunguzi wa umoja wa mataifa . Rwanda inakana madai hayo, na rais wa Rwanda Paul Kagame hakuhudhuria mkutano huo.

Mwandishi :Sekione Kitojo

Mhariri : Iddi Ismail Ssessanga