1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hotuba ya Kabila ilivyopokelewa na wananchi

20 Julai 2018

Rais Joseph Kabila wa DRC ameahidi kuheshimu katiba na kalenda ya uchaguzi. Katika hotuba yake kwa taifa alisema nchi hiyo ina uwezo wa kujisimamia yenyewe katika uchaguzi wake bila ya msaada wa nje.

https://p.dw.com/p/31oGY
Bango la Rais Joseph Kabila
Picha: DW/K. Tiassou

J2 20.07 DRC Kabila speech Analysis - MP3-Stereo

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema shinikizo zaidi linahitajika kwa haraka kumshawishi Kabila abadili mwelelekeo. Baadhi ya wataalamu wanakhofia kwamba nchi hiyo huenda ikarudi katika umwagaji damu ikiwa uchaguzi hautofanyika. Lakini je hotuba ya Kabila imetathminiwa vipi? DW imezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisasa na mtetezi wa haki za binadamu Omar Kavota kutoka Kivu na alianza kwa kuzungumzia kilichogusiwa katika hotuba ya Rais Kabila.