Hujuma dhidi ya kasri la Rais Kabila
27 Februari 2011Matangazo
Watu sita wameuwawa hii leo katika jamhuri ya kidemkrasi ya Kongo kufuatia njama ya mapinduzi.Hayo ni kwa mujibu wa viongozi wa serikali mjini Kinshasa."Tumeshuhudia njama ya kutaka kuipundua serikali"Kundi la watu waliokuwa na asilaha nzito nzito wamehujumu kasri la rais" amesema waziri wa habari Lambert Mende."Wamezuwiliwa katika kizuwizi cha mwanzo barabarani-Ameendelea kusema waziri huyo na kusisitiza hali inadhibitiwa na serikali.