Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, International Criminal Court ICC, iliasisiwa Julai 17 mwaka 1998 na baadae kuundwa rasmi 2002. Lengo likiwa ni kuwafungulia mashitaka wale ambao wamehusika na uhalifu mkubwa wa kisiasa, mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na maovu dhidi ya binaadamu. Tunaitupia jicho mahakama hiyo, utendaji wake na ikiwa kweli ni chombo chenye umuhimu na kinachohitajika.