Ruto: Vifo vya njaa vya makumi ya watu ni sawa na ugaidi
24 Aprili 2023Matangazo
Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kwamba msako kabambe utafanywa dhidi ya kile alichokiita kuwa matendo yasiyokubalika ya kidini.
Amesema hayo mnamo wakati polisi wakipata miili zaidi iliyozikwa kwenye kipande cha shamba ndani ya msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi, Pwani ya Kenya.
Polisi wamemtaja mhubiri anayeshukiwa kuwapandikisha waumini hao misimamo hiyo mikali kuwa ni Paul Mackenzie Nthenge.
Hadi kufikia sasa miili ya watu 58 imepatikana huku wengine wakiokolewa wakiwa hai, japo wakiwa hali mahututi.