1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUfaransa

Idadi ya vifo kufuatia kimbunga Chido Mayotte yafika watu 39

25 Desemba 2024

Maafisa wa Ufaransa wamesema idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Chido katika visiwa vya Mayotte imeongezeka kutoka watu 35 na kufikia watu 39.

https://p.dw.com/p/4oZJL
Uharibifu wa kimbunga Chido katika kisiwa cha Mayotte
Uharibifu wa kimbunga Chido katika kisiwa cha MayottePicha: Adrienne Surprenant/AP/picture alliance

Taarifa hiyo imetolewa siku kumi baada ya visiwa hivyo kukumbwa na kimbunga hicho. Hata hivyo mamlaka husika imesema huenda maalfu wamepoteza maisha kutokana na madhara yaliyosababishwa na dhoruba hiyo.

Mamlaka imeeleza kuwa shughuli ya kuhesabu watu waliokufa inatatizika kutokana na baadhi ya familia kuwazika ndugu zao haraka. Kasi ndogo ya kupeleka misaada visiwani humo imewakasirisha wenyeji wa Mayotte, eneo maskini lililopo chini ya himaya ya  Ufaransa.

Wakati huo huo Msumbiji, imeripoti vifo vya watu 94 vilivyotokana na kimbunga Chido wakati nchi jirani ya Malawi ikiripoti vifo 13.