1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMsumbiji

Waliokufa kutokana na kimbunga Chido Msumbiji wafika 94

23 Desemba 2024

Idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Chido nchini Msumbiji imefikia watu 94. Idadi hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kukabiliana na majanga nchini humo.

https://p.dw.com/p/4oUZM
Msumbiji | Chido | Kimbunga
Athari ya kimbunga Chido katika wilaya ya Mecufi, mkoa wa Cabo Delgado, Msumbiji.Picha: UNICEF MOZAMBIQUE/via REUTERS

Kimbunga Chido kiliipiga pwani ya Msumbiji yapata wiki moja iliyopita, japo eneo lililoathiriwa zaidi na kimbunga hicho ni visiwa vya Mayotte.

Inaarifiwa kuwa, kimbunga hicho kimefanya uharibifu mkubwa katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado. Takriban watu 620,00 wameathirika na kimbunga hicho nchini Msumbiji, wakati 500,000 kati ya hao wakiishi Cabo Delgado.

Soma pia: Kimbunga Chido chauwa watu 13 Malawi na kuwaathiri 45,000 

Wataalamu wanasema kimbunga Chido kimekuwa na nguvu zaidi kutokana na athari ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli za kibinadamu.

Jimbo la Cabo Delgado hukumbwa mara kwa mara na vimbunga vya tropiki lakini pia jimbo hilo linakabiliwa na vurugu zinazotokana na uasi wa muda mrefu.