1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF kufanyiwa mageuzi makubwa

Munira Muhammad24 Oktoba 2010

Mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi duniani G20 wamekubaliana kulifanyia mageuzi shirika la IMF

https://p.dw.com/p/PmDc
Mawaziri wa fedha wa mataifa ya G20.Picha: AP

GYEONGJU, Korea Kusini

Mawaziri wa fedha wa kundi la mataifa tajiri duniani na yale yanayoinukia kiuchumi G-20 wamefikia makubaliano ya kulifanyia mageuzi Shirika la Fedha Ulimwenguni IMF ili liyape sauti mataifa yanayoinukia kiuchumi. Mageuzi haya katika IMF yana maana India, China na mataifa mengine yatakuwa na usemi mkubwa, kushinda mataifa ya Ulaya, na kutoa sura kamili ya jinsi mambo yalivyobadilika kuhusiana na mataifa yapi yana ushawishi mkubwa.

Mataifa ya kanda ya Ulaya huenda yakawakilishwa kwenye Shirika hilo la fedha ulimwenguni, kwa kuwa ni kiti kimoja, wala sio kila taifa kuwa na mwakilishi wake. Hatua hii ilishutumiwa na Waziri wa fedha wa Ubelgiji Didier Reynders, lakini Mkurugenzi Mkuu wa IMF Dominique Straus-Kahn aliipokea hatua hiyo akisema ni wakati muhimu wa kihistoria.