1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

IMF yaidhinisha dola bilioni 1.1 kwa ajili ya Ukraine

21 Desemba 2024

Bodi kuu ya shirika la kimataifa la fedha, IMF jana Ijumaa imeidhinisha malipo ya dola bilioni 1.1 kwa ajili ya Ukraine kama sehemu ya mpango unaoendelea wa mkopo wa kusaidia bajeti ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4oRjT
DW  | Mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva
Mkuu wa shirika la kimataifa la fedha, IMF Kristalina Georgieva akizungumza na shirika la habari la DW.Picha: DW

Hatua hiyo itaisaidia Ukraine kujiimarisha katikati ya mashambulizi ya Urusi, na inachukuliwa zaidi ya mwezi mmoja tu baada ya shirika hilo kukamilisha mapitio ya sita ya mpango uliopo wa miaka minne wa thamani ya karibu dola bilioni 15.5.

Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva amesema wakati akitangaza uamuzi huo kwamba vita vya Urusi nchini Ukraine vinaendelea kuleta madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi nchini humo.

Malipo hayo yanafanya jumla ya fedha zilizotolewa chini ya mpango huo tangu uliposainiwa Machi 2023 kufikia karibu dola bilioni 9.8, kulingana na IMF.