1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India na Pakistan zakaribiana pia katika michezo:

14 Februari 2004
https://p.dw.com/p/CFgi

NEW DELHI:
Mkaribiano kati ya India na Pakistan
unajidhihirisha pia katika sekta ya mchezo wa
Cricket. Kwa mara ya mwanzo baada ya miaka 14
timu ya Cricket kutoka India itaanzisha safari
ya mashindano nchini Pakistan. Waziri Mkuu wa
India Atal Bihari Vajpayee ameunga mkono safari
hiyo baada ya kuondolewa wasi wasi kuhusu
usalama wa wachezaji, iliripoti Televisheni ya
India. Safari hiyo ya mashindano imepangwa
kufanyika baina ya Machi na April. Waziri Mkuu
Vajpayee miezi kadha iliyopita alianzisha
juhudi mpya ya mkaribiano ambayo miongoni mwa
mambo mengine inasisitiza kufunguliwa njia za
usafiri na kuanzishwa uhusiano wa kibalozi kati
ya jirani hao wawili.