1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Indonesia kutuma wanajeshi Congo-DRC

23 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEiW

Jakarta:

Indonesia inajitayarisha kutuma wanajeshi 180 katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kujiunga na jeshi la kulinda amani la umoja wa mataifa. Wanajeshi hao watachukua nafasi ya wanajeshi wengine wa Indonesia watakaoondoka baada ya kuweko Congo kwa miaka miwili.

Luteni Kanali Ahmad Yani Basuki alisema wanajeshi wake watajiunga na wenzao kutoka Bangladesh, Uruguay, Pakistan, Nepal na India mwishoni mwa mwezi ujao wa Septemba.

Kwa mara ya kwanza Indonesia ilichangia wanajeshi wa kulinda amani barani Afrika mwaka 1957, ilipojiunga na jeshi la umoja wa mataifa nchini Misri. Tangu wakati huo imechangia wanajeshi katika shughuli kadhaa za kusimamia amani za umoja huo.