1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Inter hatimaye kuibeba Serie A?

1 Machi 2021

Intermilan wanazidi kupata matumaini ya kuutilia kikomo utawala wa Juventus katika Serie A kwa kuendelea kupata matokeo mazuri.

https://p.dw.com/p/3q4Dd
Champions League | Borussia Mönchengladbach v FC Internazionale
Picha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Mwishoni mwa wiki, miamba hao waliwafunga Genoa 3-0 huku Romelu Lukaku akicheka na wavu na kusaidia kutengeneza mabao mengine mawili yaliyotiwa kimiani na wachezaji wenzake wa zamani katika klabu ya Manchester United Matteo Darmian na Alexis Sanchez.

Vijana hao wa Antonio Conte kwa sasa wako pointi nne mbele ya timu iliyo katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ya Serie A AC Milan ambao waliwafunga AS Roma 2-1.