1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran kufanya mazungumzo ya nyuklia na UIaya

28 Novemba 2024

Iran inatazamiwa kukutana na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwa mazungumzo kuhusu mpago wake wa nyuklia, baada ya serikali hizo kuungana na Marekani kutaka Tehran ikemewe na shirika la Umoja wa Mataifa la Atomiki.

https://p.dw.com/p/4nXEb
Iran Majid Takht Ravanchi
Mwanadiplomasia wa Iran Majid Takht-RavanchiPicha: Atilgan Ozdi/AA/picture alliance

Mwanadiplomasia wa Iran Majid Takht-Ravanchi, anayehudumu kama naibu wa Waziri wa Mambo ya Kigeni Abbas Araghchi, anatarajiwa kuiwakilisha Iran katika mazungumzo ya Ijumaa.

Atakutana kwanza na Enrique Mora, naibu katibu mkuu wa taasisi ya mambo ya kigeni ya Umoja wa Ulaya. Wiki iliyopita, bodi ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki - IAEA yenye mataifa 35 wanachama ilipitisha azimio la kulaani Iran kwa kukosa ushirikiano katika masuala ya nyuklia.

Iran kufanya mazungumzo ya Nyuklia na mataifa matatu ya Ulaya

Iran ililitaja kuwa lililochochewa kisiasa azimio hilo lililowasilishwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani. kwa kujibu, Tehran ilitangaza uzinduzi wa "mitambo mipya ya hali ya juu" iliyoundwa ili kuongeza hifadhi yake ya madini yaliyorutubishwa ya urani.